麥克謙聖經旅程

麥克謙一年通讀

每天 4 段經文,一年讀完舊約 1 次、新約與詩篇 2 次。

365 一年固定通讀表
4 每天 4 段經文
273 選取的日次
‹ 第 273 天 / 共 365 天 ›
譯本

讀經確認

你完成了這一天的麥琴讀經嗎?

點選確認後,會在我的頁面麥琴進度表中記錄為已完成。

家庭崇拜 · 舊約

열왕기상 2

開啟正文 →

正文尚未準備好。

家庭崇拜 · 新約

갈라디아서 6

開啟正文 →
第 6 章

Bear One Another's Burdens and Do Good

1Ndugu, kama mkimwona mtu fulani amekosea, basi, ninyi mnaoongozwa na Roho mwonyeni mtu huyo ajirekebishe; lakini fanyeni hivyo kwa upole, mkiwa na tahadhari msije nanyi wenyewe mkajaribiwa.

2Saidianeni kubeba mizigo yenu na hivyo mtatimiza sheria ya Kristo.

3Mtu akijiona kuwa ni kitu, na kumbe si kitu, huyo anajidanganya mwenyewe.

4Lakini kila mmoja na aupime vizuri mwenendo wake mwenyewe. Ukiwa mwema, basi, anaweza kuona fahari juu ya alichofanya bila kuwa na sababu ya kujilinganisha na mtu mwingine.

5Maana kila mmoja anao mzigo wake mwenyewe wa kubeba.

6Mwenye kufundishwa neno la Mungu na amshirikishe mwalimu wake riziki zake.

7Msidanganyike; Mungu hafanyiwi dhihaka. Alichopanda mtu ndicho atakachovuna.

8Apandaye katika tamaa za kidunia, atavuna humo uharibifu; lakini akipanda katika Roho, atavuna kutoka kwa Roho uzima wa milele.

9Basi, tusichoke kutenda mema; maana tusipolegea tutavuna mavuno kwa wakati wake.

10Kwa hiyo, tukiwa bado na wakati, tuwatendee watu wote mema, na hasa ndugu wa imani yetu.

Boasting Only in the Cross of Christ

11Tazameni jinsi nilivyoandika kwa herufi kubwa, kwa mkono wangu mwenyewe.

12Wale wanaotaka kuonekana wazuri kwa mambo ya mwili ndio wanaotaka kuwalazimisha ninyi mtahiriwe. Wanafanya hivyo kwa sababu moja tu: kusudi wao wenyewe wasije wakadhulumiwa kwa sababu ya msalaba wa Kristo.

13Maana, hao wenyewe waliotahiriwa hawaishiki Sheria; huwataka ninyi mtahiriwe wapate kujivunia alama hiyo mwilini mwenu.

14Lakini mimi sitajivunia kamwe chochote isipokuwa msalaba wa Bwana wetu Yesu Kristo; maana kwa njia ya msalaba huo ulimwengu umesulubiwa kwangu, nami nimesulubiwa kwa ulimwengu.

15Kutahiriwa au kutotahiriwa si kitu; cha maana ni kuwa kiumbe kipya.

16Wanaoufuata mwongozo huo nawatakia amani na huruma; amani na huruma kwa Israeli—Wateule wa Mungu.

17Basi, sasa mtu yeyote asinisumbue tena, maana alama nilizo nazo mwilini mwangu ni zile za Yesu.

18Ndugu, nawatakieni ninyi nyote neema ya Bwana wetu Kristo. Amina.

個人靈修 · 舊約/詩篇

에스겔 33

開啟正文 →

正文尚未準備好。

個人靈修 · 新約

시편 81, 82

開啟正文 →

正文尚未準備好。